Mwongozo Wa Kitaifa Wa Rufaa Ya Wagonjwa Wanaopata Huduma Za Tiba Asili Na Tiba Mbadala
Add note
Guidelines

Document was added

Jan 13 2022

Summary

Serikali ya Tanzania imejumuisha huduma za tiba asili na tiba mbadala katika Sera ya Afya kama Sehemu ya huduma za afya ya msingi inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania. Urasimishaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini Tanzania umehusisha ujumuishaji wa tiba asili na tiba mbadala katika Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 1990, na Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na. 23 ya mwaka 2002 kutungwa. Pamoja na mfumo wa kiutawala (Sehemu ya Tiba Asili ndani ya Idara ya Tiba- katika ngazi ya Wizara mwaka 1989; uanzishwaji wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala mwaka 2005; na uanzishwaji wa Waratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala katika kila Mkoa na Halmashauri) ili kuwezesha utekelezaji wa uendelezaji na ufuatiliaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala hapa nchini.

Aidha, Sera ya Afya ya Mwaka 2007 imetamka kwamba “Serikali itaandaa kanuni, miongozo na taratibu za usimamizi wa utoaji huduma za tiba asili na tiba mbadala”...