Mwongozo Wa Udhibiti Wa Ugonjwa Wa Uviko-19 Kupitia Afua Ya Kuthibiti Misongamano Katika Jamii Bila Kuathiri Shughuli Za Kiuchumi Julai 2021
Add note
Guidelines

Document was added

Jan 13 2022

Summary

Kutokana na mwenendo wa ugonjwa wa corona (UVIKO-19) nchini, Kamati ya Wataalamu imeainisha maeneo mahususi yanayohitaji kutiliwa mkazo kupitia afua za kupunguza msongamano katika jamii. Lengo ni kukata mnyororo wa maambukizi katika ngazi ya kaya na jamii. Mwongozo huu utawawezesha Wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii sambamba na kubadili tabia zao huku wakizingatia mbinu za kujikinga na ugonjwa, kwa kupata elimu ya kutosha, na kujiwekea utaratibu wa kudhibiti ugonjwa kutokusambaa kwenye jamii. Wananchi tayari wamepokea mbinu hizi kwa mtazamo chanya lakini zinahitaji kuimarishwa bila kulega lega ili jamii iweze kujikinga, kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa UVIKO- 19.