Mwongozo Wa Udhibiti Wa Maambukizi Ya Covid-19 Katika Shule Vyuo Na Taasisi Za Elimu Nchini Julai 2021
Add note
Guidelines

Document was added

Jan 13 2022

Summary

izara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW) imeendelea kufanya ufuatiliaji wa mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 nje na ndani ya nchi. Katika siku za hivi karibuni idadi ya wagonjwa imekuwa iongezeka kuashiria uwepo wa maambukizi kwenye jamii. Hivyo, wizara ya afya imedhamiria kuhamasisha jamii kuongeza kasi ya kuzingatia utekelezaji wa afua za kudhibiti na kuzua maambukizi katika maeneo yote ya kutolea huduma yakiwemo maeneo ya shule. Kwa kuwa huu ni msimu wa kufungua shule na tupo kwenye tishio ni vema afua mbalimbali zikafuatwa.

Kutokana na mahitaji mbalimbali kwa wakati wa sasa, Wizara imepitia upya Mwongozo wa udhibiti wa maambukizi ya COVID-19 katika shule, vyuo na taasisi za elimu nchini ulitolewa mwaka 2020 na ambao unaendelea kutumika hadi leo na kufanya maboresho machache. Mwongozo huu unalenga kuweka mazingira wezeshi katika maeneo ya Taasisi za elimu ikiwa ni pamoja na; Vyuo, shule za sekondari, shule za msingi, shule za awali na vituo vya kulelea watoto wadogo mchana (day care centres) kabla ya wanafunzi kurejea shuleni na vyuoni kuendelea na masomo katika kipindi hiki ambapo bado kuna mlipuko wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi aina ya Corona....